KWA NINI TUMEUMBWA?
Allah ametuumba tumuabudu yeye peke yake, na akawatuma kwetu Mitume (wajumbe wake) na akatuteremshia vitabu, ili kufafanua vipi tumuabudu yeye? Kwa hivyo atakaemuabudu Allah na kutii amri zake na kuepuka makatazo yake, atapata radhi zake. Na asiemuabudu na akakataa kutii maamrisho yake atastahiki ghadhabu na adhabu yake.