Kila sifa kamilifu zinamstahiki Allah Mtukufu, tunamtukuza na tunamuomba msaada na tunatubia kwake, na tunajilinda kwake kutokana na shari za nafsi zetu na matendo yetu mabaya, yeyote aliyeongozwa na Allah hakuna wa kumpoteza, na aliyepotezwa na Allah hakuna wa kumpoteza, nashuhudia ya kwamba hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake hana mshirika, na ninashuhudia ya kwamba Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake ni mja wake na ni Mtume wake.