Katika Hajj… hakuna mtu anayependekezwa zaidi ya mwingine.
Hakuna anayouliza: Unatoka wapi?
Hakuna anayejali una pesa kiasi gani, cheo chako kazini ni kipi, rangi ya ngozi yako ni ipi, au jina la familia yako ni nani.
Mahujaji wote huvaa mavazi yaleyale rahisi: vipande viwili vya nguo nyeupe zisizoshonwa, bila mapambo, bila chapa, bila urembo.
Mkurugenzi kutoka New York, mkulima kutoka Afrika, daktari kutoka Uturuki, mfanyakazi kutoka Asia ya Kusini…
Wote wanasimama mstari mmoja, wanatembea ardhi ile ile, wanasoma dua zile zile, na kutamani rehema ile ile.
Hakuna anayesimama juu ya mwingine.
Katika wakati huo, mwanadamu hubaki kama alivyo, bila mapambo, akisimama mbele ya Muumba wake kama alivyoumbwa mara ya kwanza.
Hajj ni onyesho kubwa zaidi la usawa na umoja duniani.
Usawa ni msingi muhimu katika Uislamu. Uislamu ulija kuonyesha kwamba watu wote ni sawa kwa asili na heshima. Hakuna aliye bora isipokuwa kwa uchamungu — sifa inayojulikana na Mungu pekee.
Allah Mtukufu anasema:
“Enyi watu! Sisi tumewaumba nyinyi kutokana na baba mmoja, naye ni Ādam, na mama mmoja, naye ni Ḥawwā’, hivyo basi hakuna kufadhilishana baina yenu kinasaba, na tumewafanya nyinyi kwa kuzaana kuwa mataifa na makabila mbalimbali ili mjuane nyinyi kwa nyinyi, hakika mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemcha Yeye zaidi. ” [Qur’an 49:13, Surah Al-Hujurat]
Na Mtume Muhammad (amani iwe juu yake) alisema:
“Enyi watu, hakika Mola wenu ni mmoja, na baba yenu ni mmoja. Hakuna ubora wa Mwarabu juu ya asiye Mwarabu, wala asiye Mwarabu juu ya Mwarabu, wala mwenye ngozi nyekundu juu ya mweusi, wala mweusi juu ya mwenye ngozi nyekundu — isipokuwa kwa uchamungu.”
[Imepokewa na Ahmad]
Hajj ni mahali ambapo tofauti zote za kibinadamu hutoweka, na umoja huzaliwa — si kwa siasa wala utajiri, bali kwa imani.
Tunaweza kutofautiana kwa mambo mengi...
Lakini katika wakati huu mtakatifu, unaona ukweli tunaousahau mara nyingi:
Kwamba kwa kiini chetu, sisi sote ni wanadamu, sawa, wa dhati, na tunapita tu katika maisha haya.
#Hajj #Usawa #UmojaWaBinadamu #chatanddecide