Uislamu ni dini ya Mitume wa Mwenyezi Mungu

Bayan AL-Islam
Shiriki:

Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa dunia na Mwenye kuiendesha dunia, na kujifungamanisha kwake kwa mapenzi na kumtukuza, na msingi wa Uislamu ni kumuamini Mwenyezi Mungu, na kuwa Yeye Mwenyezi Mungu ni Muumbaji, na kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu kimeumbwa, na kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anastahiki kuabudiwa peke yake asiye na mshirika, hakuna wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, majina mazuri yote ni yake na sifa za juu zote ni zake, na ni Mwenye ukamilifu wa
moja kwa moja bila ya upungufu, hakuzaa wala hakuzaliwa wala hakuna wa kulinganishwa naye wala kufananishwa naye, wala haingii katika kiwiliwili, na wala hajifanyi mwili wa yeyote katika viumbe wake.