Mungu Mola wa viumbe vyote, sala na amani ziwe juu ya Imamu wa Mitume, Nabii wetu Muhammad, na jamaa zake, na Masahaba wake wote. Ama baada:_
UISLAMU:_ ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja, na Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (kushuhudia) kwa moyo, na kwa ulimi, na kwa viungo.