Shiriki:
KUMUAMINI ALLAH: Muislamu anamuamini Allah Mtukufu, kwa maana ya kuwa anakubali uwepo wa Mola mlezi - utakasifu ni wake-, na kwamba yeye Mtukufu, ndiye muumba wa mbingu na ardhi, anajua vilivyojificha, na vinavyo onekana. Ni Mola Mlezi wa kila kitu na mmiliki wake.