QURANI TUKUFU na tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili

Kiwanda cha Mfalme Fahad, cha kuchapa Misahafu Mitukufu
Shiriki:

Qur'ani tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Aliiteremsha hivi ilivyo, kwa herufi zake na maana yake, kwa Mtume wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ambaye ni rehema kwa viumbe wote, mwenye kuleta bishara njema na mwenye kuonya, mwenye kuita watu waelekee kwa Mwenyezi Mungu kwa amri Yake na ambaye ni taa yenye kung'ara.